Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm ameguswa kufukuzwa kwa Dylan Kerr, kasema haya …

Ikiwa ni wiki moja imepita toka uongozi wa klabu ya Simba utangaze kuachana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, muingereza Dylan Kerr, January 18 kocha wa Dar Es Salaam Young Africans muholanzi Hans van der Pluijm amefunguka na kueleza mtazamo wake juu ya hilo, licha ya kuwa alikaa kimya.
Hans anaamini ni kweli Simba inataka kurejesha heshima yake na kuwa katika nafasi nzuri, ila kwa utamaduni na tabia ya kuendelea kufukuza makocha na benchi la ufundi kwa muda mfupi hafikirii kama itasaidia kitu chochote katika harakati ya kurejesha heshima ya timu hiyo.

Kushoto ni Dylan Kerr aliyekuwa kocha wa Simba na kulia ni kocha wa Yanga Hans van der Pluijm
“Nafahamu Simba ni timu kubwa na inataka irudi kwenye nafasi yake, lakini nafikiri haikuwa sahihi kumuondoa Kerr wakati huu, ilikuwa ni nafasi ya pekee kwa Kerr kuendelea kuisuka Simba kwa maana haikuwa na matokeo mabovu ya kusababisha kumuondoa kocha, Ila kama mtindo huu utaendelea wa kufukuza benchi la ufundi kila baada ya muda mfupi, sidhani kama Simba itakaa sawa hivi karibuni” >>>









0 comments: